Best Blogger TipsSoon

Montag, 12. September 2011

TZMPAKAAU

Msiba mwingine !!
  • Sasa ni Nairobi 
  • Mamia waripotiwa kupoteza maisha
  • Chanzo kinasemekana ni mlipuko wa bomba la mafuta
Mlipuko huo kama unavyoonekana


Mmoja kati ya majeruhi wa moto

Die Leitung explodierte in einem Armenviertel
Mmoja kati ya watu walioonekana eneo la tukio wakiwa salama lakini wenye majonzi mazito

Zaidi ya watu mia moja ishirini wamekufa baada ya bomba la mafuta kupasuka na kulipuka katika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, polisi wamesema.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la viwandani la Lunga Lunga na askari wa zima moto walipambana na moto mkali ambao ulikuwa ukitishia makazi ya watu mjini humo.
Bomba hilo la mafuta limepita katika makazi ya watu wengi kwenye mitaa ya mabanda katikati ya mji wa Nairobi na Uwanja wa ndege.
Zaidi ya majeruhi 100 wamepelekwa hospitali, maafisa wanasema.
Msemaji wa magari ya huduma za dharura alisema waathirika wengi waliungua kiasi cha kutokufatambulika.
Taarifa zinasema mlipuko huo huenda umesababishwa na kishungi cha sigara kilichotupwa katika mtaro wa maji ambao ulikuwa ukielea mafuta.
Mafuta hayo yalivuja kutoka kwenye tangi moja katika ghala linalomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Kenya, msemaji wa polisi Charles Owino ameliambia shirika la habari la Reuters.

‘Miili yaelea’


Polisi na jeshi wameweka vizuizi katika eneo hilo, ambapo wakazi walisema kuvuja kwa mafuta kwenye bomba hilo na kusababisha watu wengi kukimbilia kuchota mafuta yaliyovuja.
"Kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko, mlipuko mkubwa, na moshi na moto ukiwaka juu angani," mkazi mmoja Joseph Mwego aliliambia shirika la habari la AFP.
Baadhi ya majeruhi wakipelewa hospitali
Sehemu ya miili ilionekana ikiungua kiasi cha mita 300 (futi 1,000) karibu na eneo la tukio, wenyeji walisema.

Vyanzo:BBC,Vienna Online,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen