- Asema inanuka rushwa na inaiingizia serikali hasara
Waziri wa ujenzi ndg J.P.Magufuli
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema Kitengo cha Manunuzi makao makuu ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kinanuka kwa rushwa na kutangaza kukivunja kwa maelezo kuwa kinaendelea kuitia hasara serikali.
Alisema watumishi wa kitengo hicho wanaongeza gharama katika miradi ya ujenzi na kuongeza kwamba hivi sasa kilomita moja ya barabara inajengwa kwa Sh. bilioni 1.8 huku barabara ikiwa chini ya kiwango.
“Mheshimiwa Rais, lazima kuwepo na nidhamu katika matumizi ya fedha za serikali ili ziendane na miradi husika na sio vinginevyo,” alisema waziri Pombe Magufuli.
Waziri Magufuli anayeonekana mbele kabisa akikagua mradi mmojawapo wa barabara
Alisema serikali imedhamiria kwa dhati kuboresha sekta ya barabara nchini na kuongeza kuwa mwaka 2011/2012 wizara yake imetengewa Sh. trilioni 1.49 na kwamba fedha hizo zitaishia kwenye ujenzi wa barabara.
Huku akishangiliwa na washiriki wa mkutano huo, Dk. Magufuli alianza kutaja miradi mbalimbali ya barabara, sehemu ilipo na kila moja kuanisha inajengwa kwa kilomita ngapi.
Vyanzo :TZMPAKAAU,IPPMEDIA
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen