Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 31. August 2011

TZMPAKAAU


Ajali ya basi yaua wanane

Basi la  kampuni ya Champion lilopatwa na ajali jana

Watu wanane wamefariki dunia na wengine 53 kujeruhiwa vibaya, baada ya basi linalomilikiwa na Kampuni ya Champion kupasuka tairi la mbele kabla ya kuacha njia na kupinduka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Stephen Zelothe, aliliambia NIPASHE jana jioni kuwa basi hilo lenye namba za usajili T 763 AEQ lilikuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam.
Kamanda huyo alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 9:20 alasiri umbali wa kilomita 17 kabla ya kufika kwenye mizani ya Nala, mkoani hapa aliongeza kuwa gari hilo likiwa katika mwendo mkali lilipasuka tairi moja la mbele na kupinduka zaidi ya mara mbili.
Kamanda Zelothe alisema kuwa majeruhi 21 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati wengine wametibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.


Vyanzo:Ippmedia,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen