Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 31. August 2011

TZMPAKAAU


VINAZUILIKA !

  Unajua vifo vingi Tanzania ni vifo ambavyo vingeweza kabisa kuzuilika, lakini mimi sijui kama ni kutokujali ni nini sielewi lakini  vifo vinatokea tena na tena na tena na hakuna hatua  zinazochukuliwa ili kuepusha.
  •     Vifo vya ajali za magari vinavyotokana na  magari kuruhusiwa kutembea huku ni mabovu,au ajali zinazotokana na madereva walevi au  madereva wasio na leseni zinazotambulika ,au barabara zilizokosa alama elekezi au barabara zenye mashimo yanayowezwa kabisa kufanyiwa ukarabati ni vingi mno na hivi ni vifo vinavyoweza  kuzuilika kabisa vinazuilika lakini tatizo ni nini?akili alizotupatia mwenyezi kweli ndio hizi au ?.Uwezo tunao ,nguvu tunazo, na sababu tunazo kuchukua hatua.

  • Vifo vinavyotokea mahosptalini kwasababu tu wauguzi walitaka rushwa toka kwa mgonjwa na hawakuipata jamani jamani kweli utu wetu tumeuacha wapi?  au wauguzi waliokosa sifa lakini kwa kupitia njia za panya sasa ndio tuliowaachia dhamana za maisha yetu, hakika sisi ni waungwana kuliko kondoo. Au vifo vinavyotokana na maslahi duni ya wauguzi na ukosefu wa vitendea kazi mahosptalini jamani ni nini kibaya kipo akilini mwetu au ni nini kizuri kinakosekana akilini mwetu?yaani mtu anaona ni bora anunue silaha lakini abaki na afya mbovu kweli hapa kunatatizo linalotakiwa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo.

  • Vifo vinavyotokana na kutokuzingatiwa kwa haki za binaadamu au kukiukwa kwa haki hizi.Yaani askari anaamua kuondoa uhai wa mwenzake kwasababu tu yeye ana silaha kweli ....hivi mwisho wa haya mambo ni nini?  ,au raia wenye hasira kali na waliochoka na vyombo vya dola dhalimu wanaamua kumtuhumu mtu kuwa ni mwizi wa kuku etc na wanamshtaki kisha kumwandikia adhabu ya kifo na kuitekeleza kweli tunaelekea wapi je uungwana huu tumejifunza toka kwa nani?Halafu achilia mbali wageni wanaomiliki migodi,mashamba n.k jinsi wanavyowaonea wananchi na wengine wamediriki kuwachoma moto hadi kufa wazawa...si mlisikia kilichotokea kule mji mwema na kwingineko....mabadiliko ya haraka sasa sio ombi ni lazima kabla taifa halijateketea.

Vyanzo:TZMPAKAAU,Youtube

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen