Best Blogger TipsSoon

Freitag, 22. Juli 2011

TZMPAKAAU

Wizara ya nishati na madini sasa hapakaliki
  • Katibu apewa likizo kwa kipindi kisichojulikana kupisha uchunguzi
  • Na bajeti yake imekewa kizuizi bungeni
  • Mgao wa umeme na  migogoro ya  madini vyaiponza 
Sakata la kukusanya fedha kulainisha upitishwaji wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2011/12 linalomkabili Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, David Jairo, limeingia hatua mpya baada ya kulazimishwa kwenda likizo kupisha uchunguzi ufanyike.

                                                  Philemon Luhanjo (kulia)katibu mkuu kiongozi

Maamuzi ya kumtaka Jairo aliyeziandikia taasisi zilizoko chini ya wizara yake barua akizitaka kuchangia Sh. milioni 50 kila moja ili zitumike kufanikisha mawasilisho ya bajeti hiyo, aende likizo yalitangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwenye mkutano na waandishi wa habari jana mjini hapa.


                                    Bwana Jairo katibu aliyekuwa katibu wa wizara hiyo

Hii inafuatia hatua iliyochukuliwa na bunge la jamhuri ya muungano kupinga upitishwaji wa bajeti ya wizara hiyo wiki iliyopita, kutokana na mapungufu mengi yaliyojitokeza wakati wa uwasilishaji wa bajeti hiyo na kupungua kwa ufanisi wa wizara hiyo hasa kutokana na kushindwa kulishughulikia suala la mgao wa umeme na migogoro ya madini iliyoenea nchi nzima.


Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen