Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 23. Juni 2011

TZMPAKAAU

 Lissu aja na hoja kama ile ya Kenya
  • Ni kuhusu kukatwa kodi katika posho za watumishi wa umma
  • Hoja yake yaibua kizaa zaa bungeni
  • Nimrodi Mkono,Wiliam Lukuvi ,George Simbachamweni,Jennista Muhagama na Peter Serukamba wote kutoka CCM waipinga hoja


Tundu lissu mwenye suti nyeusi akiwa amenyanyuliwa na mashabiki wake

 Lissu aliwasilisha mapendekezo ya kubadili muswada wa sheria ya fedha ya mwaka 2011/12 kwa kufuta kifungu kilichokuwa kinapendekeza posho zote wanazopewa watumishi wa serikali zisitozwe kodi, kwa kuwa ni kinyume cha mkakati wa serikali wa kuachana na matumzi makubwa yasiyokuwa ya msingi kama ilivyoanishwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano.


Lissu alifafanua kuwa kuendelea kuwasamehe kodi ya mapato watumishi hao, ni sawa na kuzidi kuwaongezea walichonacho, na si kuwaangalia wale wa kipato cha chini kwa sababu watumishi wa chini hakuna anayelipwa posho inayofikia Sh. 100,000 ambacho ndicho kima cha kuanza kukatwa kodi kisheria.

Mmoja kati ya wapinzani wengi wa hoja hiyo Mbunge wa Kigoma mjini Peter Serukamba

Mbunge wa peramiho CCM Jenista Muhagama


Pandekezo la Lissu lilipingwa na wabunge kadhaa, akiwamo Jenista Muhagama (Peramiho- CCM), George Simbachaweni (Kibakwe-CCM), Nimrod Mkono (Musoma Vijijini - CCM), Peter Serukamba (Kigoma Mjini – CCM), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, wote wakipinga mapendekezo hayo.


Waziri wa Nchi  William Lukuvi



Tofauti na wenzake, Lukuvi alisema kuwa mawazo ya Lissu ni chanya kulingana na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa serikali, lakini ni vema kukawa na utaratibu mpana wa kuchambua makundi mbalimbali katika jamii na si kuibuka tu na msimamo wa kukurupuka kama ambavyo inapendekezwa na Lissu kwa sababu madhara yake yanaweza kuwa mabaya zaidi kwa watumishi wengine.

Nimrodi Mkono akiteta jambo na rais

Moto wa mabishano ulizidi kuwaka baada ya Mkono kusema kwamba mapendezo ya Lissu yangewaumiza madiwani ambao wanalipwa posho lakini hawana mishahara.

Zitto kabwe kulia kama anavyoonekana na mama yake bi Shida Salumu

Kutokana na kauli ya Mkono, mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alisimama na kueleza kuwa kinachozungumzwa na baadhi ya wabunge kuwa msamaha huo wa kodi unawasadia watu wa kipato cha chini, wakiwamo walimu, madiwani, askari polisi na kada nyingine za chini, si za kweli kwa sababu katika kundi hilo hakuna anayelipwa posho ya Sh. 100,000 na zaidi kwani posho hii ndiyo inayopendekezwa ikatwe kodi.

Zitto alisema kuwa msamaha huo utawasaidia na kuwanufaisha zaidi wakubwa serikalini, wakiwamo mawaziri, makatibu wakuu na hata wabunge ambao tayari wana mapato makubwa wakilinganishwa na watumishi wengine.

Lissu alihitimisha hoja yake kwa kusema kuwa kimsingi hakuna ufanisi wowote utakaopatikana kwa kukataa kulipa kodi kwa kuwa wanaolengwa ni wakubwa ambao tayari wana mapato makubwa.

Vyanzo:TZMPAKAAU,IPPMEDIA

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen