Best Blogger TipsSoon

Samstag, 14. Mai 2011

TZMPAKAAU

 ZITTO KABWE:SERIKALI IMEFILISIKA
  • Yaanza kuzikopa benki za ndani
  • Madeni yake yaongezeka mara dufu
  • Wafanyakazi wake wacheleweshewa mishahara
  • Kodi kuongezwa siku za usoni
Mbunge wa kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akihutubu

Zitto, ambaye  ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2009/10, imeeleza kuwa hali   kwa sasa ni ya kutisha .

Alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG, kumekuwa na ongezeko kubwa la deni la taifa Juni 30, mwaka jana kwa kiasi cha Sh. trilioni 2.8 kwa kuwa deni hilo kwa mwaka wa fedha wa 2008/09 lilikuwa Sh. trilioni 7.6, lakini sasa limefikia Sh. trilioni 10.

“Deni hilo ni sawa na asilimia 38 zaidi ya deni la mwaka uliopita kwa mujibu wa CAG. Kama hali itaendelea kuwa hivi, tutaumia sana” alisema Zitto.

Alisema hali hii inamfanya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuwa “Waziri wa madeni” kwa kuwa tangu ashike Wizara hiyo, deni la taifa limekuwa likipanda kila mwaka.
Waziri wa fedha Mustapha Mkulo kama anavyoonekana.

“Huu ni mzigo mkubwa kwa wananchi. Sisi tunapambana kutaka kodi ipunguzwe. Lakini ili serikali ilipe au kupunguza deni hili, itabidi ipandishe kodi. Kitu hicho ni manyanyaso makubwa kwa wananchi hawa masikini,” alisema Zitto.
       
Twin towers as they call them  is the Central Bank of Tanzania (BOT)

Akizungumza kwa njia ya simu jana akiwa wilayani Songea, Zitto alisema kwa miaka miwili serikali imeshakopa zaidi ya Sh. trilioni mbili katika benki za ndani.

Alisema kauli iliyotolewa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, kuwa serikali ina fedha zinazotosha kuwalipa mishahara watumishi wake haina ukweli  

“Msisikilize kauli ya Mkulo tu, nendeni mkaulize watumishi wa serikali walilipwa mishahara tarehe ngapi, sisi wabunge kwa kawaida tunalipwa mishahara tarehe 25 ya mwezi, lakini safari hii tumelipwa tarehe saba, hata halmashauri nyingi fungu wanalopata kutoka Hazina limepungua kwa kiwango kikubwa, hilo wala halina shaka ushahidi upo nendeni mkaulize, ” alisema. Zitto alisema ana ushahidi wa baadhi ya halmashauri kupewa kiasi kidogo sana cha fedha kuliko kiwango kilichopangwa kwa halmashauri hizo kila mwaka.

“Halmashauri ya wilaya ya Ludewa imepewa asilimia 43 tu ya fedha ambazo walipaswa kupata, halmashauri ya wilaya ya Kigoma wamepewa asilimia 47 ya fedha walizopaswa kupewa kutoka Hazina, sisi mkoa mzima wa Kigoma tumepatiwa asilimia 53 tu ya fedha zilizopaswa kutolewa sasa wanataka ushahidi wa aina gani kuthibitisha kuwa serikali imefikisika,” alihoji Zitto. Alisema kodi ya ushuru wa forodha ndiyo pekee inaonekana kuongezeka kwa sababu ya mafuta yanayoingizwa nchini, lakini kodi za ndani makusanyo yameshuka kwa kiwango kikubwa.
Bossi wa Tanzania Revenue Authority TRA Mr.Harry Kitilya akielezea jambo.


Alisema TRA imepoteza mapato ya zaidi ya Sh. bilioni 840 kutokana na tatizo la mgawo wa umeme kuanzia Januari mwaka huu hadi sasa. “Hii taarifa imetolewa na TRA wenyewe siyo yangu, wenyewe ndio wametamka, lakini mtu akisema wanakimbilia kukanusha, sasa wanakopa kila benki na kinachosikitisha hawakopi kwa ajili ya miradi ya maendeleo wanakopa kwa ajili ya kulipa mishahara ya wafanyakazi,” alisema Zitto.

Source:IPPMEDIA,TZMAPAAU


Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen