Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 26. Mai 2011

TZMPAKAAU

                               BUSARA ZA BURE TOKA TGNP



  • Bajeti  ilenge maendeleo ya  wananchi si ya wawekezaji







  •  


    SERIKALI imetakiwa kuhakikisha kwamba mwongozo wa bajeti ya miaka mitano (2011/12 – 2015/16) unalenga kujenga uchumi ambao utajenga maisha ya watu wake kwanza na si kuangalia maslahi ya wawekezaji wa ndani na nje.


    Mkurugenzi mtendaji wa TGNP mama Usu Mallya



    Hayo yamo katika taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupitia kikundi-kazi chake na wanaharakati wengine kuhusu uchambuzi wake wa muongozo wa mpango wa miaka mitano wa bajeti kwa mwaka wa fedha utakaoanza Julai mwaka 2011/2012 hadi 2015/16 .

    Mwongozo wa bajeti ni lazima ulenge namna uchumi wa nchi utakavyojenga maisha ya watu wake kwanza na si kuangalia tu wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Suala la ajira na maisha endelevu kwa wote liwekewe kipaumbele,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kwamba masharti yawekwe kwa wawekezaji  (awe wa ndani au nje)  kwamba  aongeze idadi ya wafanyakazi wa ndani  kwa asilimia kadhaa kufuatana na ukuaji wa sekta husika.





    Vipaumbele vilivyoainishwa katika muongozo huo wa bajeti inayopendekezwa na TGNP ni 
    • Kilimo
    • Uwekezaji katika rasilimali watu
    • Mazingira endelevu
    • Usimamizi wa ardhi
    • Mipango miji na makazi
    • Kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na sekta binafsi
    Mambo mengine yaliyotajwa katika taarifa hiyo ni pamoja na kuongeza bajeti katika elimu, huduma za bure kwa kina mama wajawazito na vivutio kwa wafanyakazi katika sekta ya afya.

    “Mikakati ya kuinua soko la bidhaa za ndani kwa kuimarisha barabara za vijijini zitakazosaidia kuchukua mazao ya wakulima wadogo wadogo ambapo wengi wao ni wanawake, yote hii katika kuinua pato la ndani la taifa na kuimarisha uchumi mkuu,” inasema taarifa hiyo na kuongeza ulazima wa kuchukuliwa   mikakati maalum ya kuongeza ajira, maisha endelevu na kipato kwa wote, wanawake na wanaume, mijini na vijijini.

    Hii ni busara ya bure kabisa kwa serikali watendaji wake na kwa wananchi wa kawaida toka kwa hawa wanaharakati wa TGNP

    keyword: Tanzania Gender Networking Programme(TGNP)

    Vyanzo:TZMPAKAAU,Globalpublishers

    Keine Kommentare:

    Kommentar veröffentlichen