Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 19. Mai 2011

TZMPAKAAU

  TARIME HAPAKALIKI
  • Ni kufuatia mauaji ya wananchi katika mgodi wa North Mara                   
  •   Mbuge afurumshwa kwa mawe
  • Sare za CCM zachanwa
Uzalishaji ukiendeleakatika mgodi wa North Mara
Hali katika kitongoji cha Nyamongo ni tete ikichangiwa na hisia kali za vifo vya watu watano waliouawa na Polisi kwa madai ya kutaka kuvamia mgodi wa North Mara.

Na sasa Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwene (CCM) na viongozi wengine wa halmashauri ya wilaya ya Tarime wameshambuliwa kwa mawe na magari yao kuharibiwa vibaya.


Mbunge wa Mara Nyambari Nyangwine

Tukio hilo lilitokea jana wakati Nyangwene akiwa na msafarawake wakiwasili Nyamongo katika mkutano uliokuwa umeitishwa kuzungumzia tukio la mauaji hayo, lakini miongoni mwa waliokuwamo kwenye msafara huo ni makada wa CCM waliokuwa wamevaa sare za chama hicho, hali iliyoamsha taharuki kubwa.



Katika kadhia hiyo, kada mmoja wa CCM ambaye jina lake halikupatika mara moja, shati lake la chama lilichanwa chanwa, huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime, Amos Sagana, akivua sare ya shati na kofia za CCM na kubaki na fulana tu.


Makada wengine wa CCM aliokuwa wamevaa sare hizo, walilazimika kuzivua na kujisalimisha kwenye ofisi ya serikali ya mtaa katika eneo hilo.

Magari yaliyoharibiwa kwa kuvunjwa vioo ni la mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime, Toyota Land Cruiser namba STK 8411 na la waandishi wa habari T299 ASW aina ya Toyota Land Cruser Prado mali ya mbunge huyo.

Yote yalipigwa kwa mawe yaliyokuwa yakirushwa mfululizo na wananchi jambo lilisababisha mbunge huyo na msafara wake kukimbia huku wakiendelea kushambuliwa.

Wananchi hao walieleza pia kwamba kitendo cha serikali kushindwa kuwapatia maeneo ya wachimbaji wadogo wadogo pamoja na kushindwa kuchukua hatua za haraka katika kudhibiti mauaji ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakifanywa na polisi katika mgodi wa dhahabu wa North Mara ni moja ya sababu za kufanya hivyo.


“Sisi hatuna shida na mbunge wetu kwanza yeye hakuua, lakini hatuwezi kumsikiliza kwa vile serikali yake ndio inayotumia polisi kulinda Wazungu na kutuua sisi kinyama kila kukicha,” alisema mwananchi mmoja.

Mwananchi mwingine alijitambilisha kwa jina la Chacha Keresa, alisema viongozi wa serikali katika ngazi ya wilaya wamekuwa wakishindwa kutatua matatizo yao, lakini wamekuwa wakijitokeza hadharani pindi tu wanaposikia wananchi wanakusudia kuwafanyia fujo wawekezaji.


“Siku zote sisi tunasema hatuna eneo la kulima tunataka tupewe sehemu ya kufanya uchimbaji mdogo, lakini umekuwa wimbo sasa leo wameuawa vijana wetu tena hata maiti zikiwa bado hazijazikwa wanakuja na nguo za CCM kufanya nini,” alisema.

Makada wa chama tawala

Naye Yahana Chacha, alisema endapo serikali haitachukua hatua za haraka za kutatua tatizo la umaskini linalowakabili wananchi wa maeneo hayo hakuna amani itakayopatikana daima.
“Tunachosema hakuna jambazi anayekwenda kuiba mawe haya yote tunayafanya kwa umaskini sasa hapa si kutumia polisi bali serikali itafute njia ya kumaliza umaskini kwa wananchi bila hivyo wataleta hata JWTZ lakini hakuna watakachosaidia,” alisema.

Mbunge wa Tarime na mwandishi wa vijitabu aliyasema haya baada ya kuponea chupuchupu

“Natumia nafasi hii kuitaka serikali licha ya kuchukua hatua kwa wote waliohusika na mauji haya ya wananchi, lakini pia serikali kupitia Wizara ya Nishati itekeleze kwa vitendo mpango wa kuwapatia wananchi maeneo ya kuchimba na wawekezaji watekeleze kwa vitendo makubaliano yaliomo katika mikataba,” alisema Nyangwine.

Vyanzo :TZMPAKAAU,IPPMEDIA

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen