Best Blogger TipsSoon

Samstag, 9. April 2011

TZMPAKAAU

Warioba anena!!
  • Ni katika mjadala wa Muswada wa Katiba mpya
Ataka kila kitu kijadiliwe kupata kwa uwazi
Imeelezwa kuwa itakuwa si sahihi kuwazuia Watanzania kuhoji baadhi ya masuala ya msingi hata kama tayari yapo katika katiba ya sasa, kwani ni bora yakajadiliwa kwa kina ili yajulikane kama yanakidhi mahitaji ya watu kujitawala au la.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na mmoja wa viongozi waandamizi wastaafu nchini, Jaji Joseph Warioba, wakati akitoa maoni yake katika kuboresha muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba, akisisitiza kuwa masuala yaliyoko sehemu ya 3, kifungu cha 9(2), yajadiliwe bila zuio lolote.

Kifungu hicho cha muswada, kinataja mambo 8 ambayo ni marufuku watu kuyahoji au kuyazungumzia wakati tume ya kukusanya maoni ya watu juu ya katiba mpya itakapokuwa ikitekeleza majukumu yake.

Masuala hayo yanayoitwa kuwa ya 'heshima na utukufu', hivyo hayapaswi kuguswa kwa maslahi ya taifa, yameainishwa katika muswada kama ifuatavyo; Kuwepo kwa Muungano wa Tanzania na Zanzibar, kuwepo kwa mihimili mitatu ya dola (bunge, serikali na mahakama), nafasi ya urais, mshikamano wa kitaifa na amani ya nchi.

Mengine ni; kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuwepo kwa mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia, haki za binadamu, dhana ya utu wa mtu, usawa mbele ya sheria na mfumo unaoweka utaratibu wa kufuata sheria, dhana ya Serikali ya Tanzania kutokuwa na dini na uhuru wa mahakama.

"Haya mambo yanayoitwa matakatifu na hivyo hayaguswi ndiyo katiba yenyewe, ndiyo mambo ya muhimu katika katiba huwezi kuyaondoa watu wasiyazungumze...lazima watu wayazungumze hata kama tayari yako katika katiba ya sasa. Msiwazuie watu kusema, aliongeza. kwa habari zaidi tembelea

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen