Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 13. April 2011

TZMPAKAAU

Maneno ya mwisho ya Makamba


Aliyekuwa katibu mkuu wa CCM taifa bw.Yusuph Makamba


Katibu mkuu mpya wa CCM bw.Wilson Mukama mwenye mawani  akielezea jambo


 Bw. Yusuph Makamba amewataka Watanzania na wanachama wa CCM wasifadhaike kwa kujiuzulu kwao kwani 'wanarudi kwa baba ambaye amewaletea mtume mwingine'.Haya aliyasema alipopewa nafasi ya kuaga rasmi kwa niaba ya sekretarieti iliyoenguka madarakani.

Mbali na hilo, Bw. Makamba alionesha furaha yake kwa kutowajibika peke yake,
“Nashukuru tumetoka wote, kama tulivyoingia pamoja na tunatoka pamoja tukiwa wamoja. Haiwezekani mmoja anyoshewe kidole. Hata baadhi ya wajumbe wa mkutano huu walisema atoke Makamba, mimi nikasema tutoke wote”.


 Kwa kutumia misemo ya biblia, Bw. Makamba alisema wanarudi kwa baba yao kutayarisha makao mapya na hata wenzao waliokuja na kukalia viti walivyoviacha watawakuta huko.
 "Baba ameleta mfariji mwingine ambaye ni Wilson Mukama na wajumbe wengine. Wanachama tuendelee kuvumiliana na kujipanga ili kupata ushindi mkubwa mwaka 2015.

"Tulipoteuliwa tuliaminiwa kufanya kazi za chama na tukafanya kazi hizo kikamilifu na chama kikapata ushindi. Ndiyo, tulishinda hata kama ni kwa namna gani, lakini tulishinda, alisema.

Alisema wao wamekubali kumwaga damu kuokoa chama, kwani hawana tofauti sana na waliobaki na kwamba amefurahi kuona wengine nao wakichukua nafasi zao na kuwaasa kwamba wakitaka kutumia fagio la zamani wao wako tayari wakati wote, lakini wasipolihitaji wakiharibu watawasema.


Akizungumzia hulka ya yake ya kauli za kuudhi, alisema kwa mifano na kusisitiza kuwa kama unatukanwa na mtu mdogo aliyetumwa na mtu mzima ili kuweka mambo sawa, na yeye anamtukana kwa lengo la kusawazisha ili iwe sare.


Kutokana hatua hiyo, Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho imewateau Bw. Wilson Mukama amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Makamba, akisaidiwa na Naibu Makatibu Wakuu (Bara na Visiwani), Bw. John Chiligati na Bw. Vuai Ali Vuai. Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi ni Bw. Nape Nnauye, huku, Bw. Mwigulu Mchemba akichaguliwa kuongoza Idara ya Fedha na Uchumi. Mkuu wa Oganaizesheni ni Bi. Asha Abdallah Juma na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Bw. Januari Makamba.


Kwahabari zaidi soma: blog ya Majira
Vyanzo:Majira,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen