Best Blogger TipsSoon

Freitag, 8. April 2011

TZMPAKAAU

Ugomvi wa Ardhi wazua maafa dar
           

Angalizo:video ina picha zinazostua
  NOTE  :The video contains frightening scenes




  • Nyumba saba za bomolewa
  • Watu wawili wapoteza maisha
Mapigano makali ya kugombea ardhi yamezuka katika eneo la Nakalekwa Wazo Hill, jijini Dar es Salaam kati ya wakazi wa eneo hilo na mabaunsa wanaodaiwa kukodishwa kutoka Kinondoni ambapo inadaiwa watu watano waliuawa na wengine saba kujeruhiwa vibaya.
Mabaunsa hao wanadaiwa kukodishwa kwa lengo la kwenda kubomoa nyumba za wananchi hao kwa madai kuwa walivamia eneo la mtu mwingine na kujenga.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyella, alisema waliokufa ni watu wawili tu.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4:00 asubuhi na taarifa za awali zilisema kuwa mabaunsa hao waliuawa baada ya wananchi kuitana na kuwazingira na kuanza kuwashambulia kwa kutumia mikuki, marungu, pinde, mapanga na silaha nyingine za jadi.
Eneo hilo lipo katika Kata ya Wazo Manispaa ya Kinondoni jijini Dare es Salaam ambako zaidi ya wakazi 1,000 wanaishi hapo tangu mwaka 2006 baada ya kuvamia eneo la Daniel Chacha na kuamua kujenga nyumba kwa madai kuwa walilikuta likiwa pori.
Mmoja wa marehemu hao ambaye alikuwa ni baunsa akizungumza muda mfupi kabla ya kukata roho, alisema walitumwa na kampuni moja ya udalali (jina tunalihifadhi) kwa ajili ya kwenda kuvunja nyumba zilizojengwa eneo hilo kwa ujira wa Sh. 50,000 kila mmoja.
Kundi la wananchi baada ya kubaini kuwa baunsa huyo alikuwa hajafa, lilimvamia tena na kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na hatimaye akafariki dunia.
Eneo hilo jana liligeuka uwanja wa vita huku damu na nguo za marehemu na majeruhi zikiwa zimetapakaa maeneo mbalimbali.
Kwa habari zaidi tembelea ippmedia au issamichuzi.blogspot.com

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen