Best Blogger TipsSoon

Samstag, 19. März 2011

TZMPAKAAU

Libya kuweza kuchukuliwa hatua kali zaidi ikiwemo uvamizi wa kijeshi
Mataifa yaliyoahidi kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa, linalokataza ndege kuruka katika anga ya Libya, yanakutana mjini Paris, kujadili hatua ya kuchukua.
Ndege za kivita za Mataifa ya Magharibi
Ndege za kivita za Mataifa ya Magharibi

Viongozi wa Ufaransa, Ungereza na Marekani, wamejumuika na nchi za Jumuiya ya Kiarabu, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon.

Huku ndege za kijeshi zinapelekwa eneo la Mediterranean, Kanali Gaddafi, ameonya Mataifa ya Magharibi, yatajuta, endapo yataingilia kati.

Taarifa yake imesema, azimio la Umoja wa Mataifa, linatoa idhini ya kuingilia kati kijeshi, sio halali.
Mwakilishi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, amesema, anatarajia hatua za kijeshi, zitaanza katika saa chache baada ya mkutano huo wa Paris.



Hotuba ya Obama jana juu ya hali ya Libya
Katika hatua nyengine Gadafi amemuandikia rais wa marekani  barua leo , akimueleza kuwa Libya kamwe haikabiliani  raia wake  kijeshi, isipokuwa Libya inachokifanya ni kukabiliana na magaidi wa Al qaeda walioivamia. Na akamuuliza Barack Obama ,je Rais huyo wa marekani angechukua hatua gani iwapo marekani kusini ingevamiwa na kuanza kumilikiwa na magaidi ?Hakuishia hapo lakini amesema anamchukulia Obama kama mtoto wake na ataendelea kumchukulia hivyo.Hii inafuatia wito uliotolewa jana na Obama ukimtaka Rais huyo kusitisha mara moja mashambulizi ya anga dhidi ya wananchi wake huku akimtaka rais huyo arejeshe maji,umeme na miundo mbinu mengine kwa wananchi wake walioathirika la sivyo hatua zitachukuliwa dhidi yake.










Wakati huo huo leo Gadafi ameandika barua kwa waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akiwataka kuacha kuingilia mambo ya ndani ya Libya.Na mwisho akieleza iwapo wawili hao wataivamia Libya basi watajutia maamuzi yao katika siku za usoni.




Katika hatua nyengine kuna uwezekano wa Libya kuvamiwa kijeshi saa yeyote ile kwani kwa taarifa zilizopatikana ndege za mataifa washiriki ya (NATO) nyingi zimeshasogeswa katika military bases za nchi majirani na Libya na waingereza wakieleza kuwa ndege zao zitawezakuruka moja kwa moja kutoka nchini kwao.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen