Best Blogger TipsSoon

Dienstag, 22. Februar 2011

TZMPAKAAU

 JWTZ na wananchi nani ahame dar?

SAA 2.30 hadi 4,30 usiku wa kuamkia Alhamisi wabongo wakageuka wakimbizi wa muda.
Wakaacha majumba yao wakakimbia kunusuru roho zao. Majumba waliyojenga kwa mamilioni ya fedha yakaonekana si chochote wala lolote mbele ya roho ambayo mwanadamu anapewa na Mwenyezi Mungu tu.
Roho huwezi kuitafuta sehemu yoyote ile, ni zawadi kutoka kwa Mungu, ikitoka hairudi; lakini fedha itatafutwa na majumba yatajengwa mengine mazuri kuzidi hayo yaliyosimama sasa hivi.
Kama ndivyo hivyo kwa nini sasa nyie majirani mnagombania kipande kidogo tu cha ardhi eti cha kwangu ohoo cha kwangu! Hadi mnaharibiana ujirani. Kwa nini msitangulize ubinadamu kwanza badala ya mali zinazotafutwa?
Katika ukimbizi huo watu wakatanguliza ubinadamu wakazoana kusikoeleweka. Ndugu zangu wa Gongo la Mboto, Pugu, Majohe, Kitunda, Mzambarauni, Ukonga, Mwembe Madafu, Ulongoni, Mongo la Ndege, Kinyerezi, Segerea, Banana, Majumba Sita, Yombo, Mazizini na
Uwanja wa Ndege wana simulizi lisiloisha.
Hao ukiwauliza usiku huo kamwe hawawezi kuusahau katika maisha yao. Siku ambayo walipoteza ndugu, watoto, wake na waume zao. Wakakimbia wasikokujua ila walikotoka wanakufahamu.
Watu wanatoka Pugu kituo cha kwanza ni Mbagala eti kunusuru roho yake. Mabomu nayo yakawafuata huko huko. Hayana huruma kwamba umetembea umbali mrefu yakusamehe.
Watu wakakimbia na wakajaza familia zao kwenye magari, misongano ikawa mirefu, magari ni nini bwana? Ni mali tu inatafutwa hiyo…watu baada ya kutafakari kwa kina wakayatelekeza magari yao na kukimbia na familia zao kuponyesha roho zao.
Hiyo ndio adha ya Dar, Jiji linalotamaniwa na kila mtizedi aje kuishi hapa. Kumbe ni Jiji ambalo limezungukwa na kambi za Jeshi, sio Jiji salama kwa raia kuishi. Ni heri tuliachie Jeshi lijivinjari lenyewe hapa Dar sisi twende mikoani.
Usibishe hebu kwa haraka haraka tu hesabu kambi hizo, anzia Gongo la Mboto, Air Wing, Mgulani, Makongo, Lugalo, Mlalakuwa, Mbweni, Kigamboni, Mbagala na Makao Makuu ya Jeshi kote huko kuna kambi za Jeshi.
Kwa mantiki hiyo Bongo yote imezungukwa na mabomu ya Jeshi! Halafu tunachekelea kuishi kwenye Jiji hili lenye hatari ya namna hii. Lini umeona watu wakaacha nyumba zao alizojenga kwa mapesa mengi kama sio mabomu ya Gongo la Mboto?
Ndio maana nasema umefika wakati Serikali yetu itafakari, aidha kuwahamisha raia wote waondoke Dar au kuzihamisha kambi hizo za Jeshi na kuzipeleka sehemu nyingine.
La sivyo utaendelea kuwa wakimbizi mara mabomu hayo yakikasirika kukaa huko yaliko kwa muda mrefu bila kutumika.
Si unajua tena hayajatumika miaka mingi, tangu vita ya Idd Amini hivyo yana hasira. Ndio maana yanaamua tu yanalipuka bila hata kuwataarifu mabosi waliyoyahifadhi kwenye hayo maghala.
Jamani JWTZ kwa hili wananchi wamewalaani sana. Wamewalaani kulipuka kwa mabomu ikiwa ni mara ya pili ndani ya miaka miwili. Ukiacha Mbagala sasa Gongo la Mboto. Nini kifanyike?
Wanahoji hivi ripoti ya ile Tume ilitoa mapendekezo gani? Ili hali hiyo ya mabomu kulipuka isijirudie? Ama ni Tume feki ambayo ilitoa mapendekezo ambayo hayatekelezeki?
Aibu hii hadi lini? Hadi mabomu yanakasirika na kuondoa roho za watu ambao hawana hatia, nani wa kulaumiwa? Dk. Mwinyi, Luteni Jenerali Shimbo au Jenerali Mwamunyange?
Mimi sina jibu ila nasema adha tuliyoipata inatosha na tuwajibike kwa hili.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen