WATUMISHI WAANZISHA MFUKO KWA AJILI YA MAENDELEO NA MAMBO YA DHARURA
Watumishi wa kata ya Naisinyai Wilaya ya Simnjiro Mkoani Manyara wameanzisha mfuko wakujikimu wenye shilingi 840,000 utakaowasaidia kwenye shughuli zao za maendeleo na wakiwa matatizoni. Wakizungumza juzi mbele ya Diwani wa kata hiyo,Kilempu Ole Kinoka watumishi hao walidai kuwa mfuko huo utakuwa endelevu na utawasaidia watumishi wakiwa katika matatizo yoyote yatakayojitoka ghafla.Walisema wameazimia kila siku ya jumamosi ya kwanza ya mwezi wawe wanakutana na kuchangia asilimia fulani ya mishahara yao kwa ajili ya kuwapunguzia ukali wa maisha uliopo hivi sasa sehemu tofauti hapa nchini.
Vyanzo:TZMPAKAAU na FullShangwe
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen