Kanisa la Tanzania Assemblies of God lililochomwa moto mtaa wa kariakoo huko Unguja
Gari la mchungaji Dickson Maganga lilichomwa moto pia
Kikosi cha kuzuia ghasia FFU kikiweka doria maeneo ya michenzani
Waandamanaji wa jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislam(JUMIKI)
Vurugu hizo zilianza baada ya wana JUMIKI kufanya maandamano, maandamano hayo yanafuatia kitendo cha kukamatwa kwa kiongozi mmoja wa jumuiya hiyo.Akitoa tamko la serikali kufuatia vurugu hizo waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohamed Aboud Mohamed amesema kuanzia sasa mikusanyiko yoyote imepigwa marufuku na kuahidi kuwatafuta na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliosababisha vurugu na kuleta uharibifu wa mali.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Michuzi na Globalpublishers
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen