NCHI SASA KUPUNGUZA MATUMIZI YA DOLA(TANZANIA TO TAKE AUSTERITY MEASURES OVER THE U.S DOLLAR)
Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, amesema serikali itaanza kutekeleza mkakati wa kulinda thamani ya Shilingi ya Tanzania ambayo imekuwa ikiporomoka thamani yake.
Dk. Mgimwa amesema kuwa alisema Wizara yake inakuja na mkakati mpya wa kuhakikisha kwamba matumizi yote ya fedha na mahitaji ya nchi yanafanyika kwa Shilingi ya za Tanzania badala ya Dola ya Marekani ili kuliepusha taifa kuendelea kuathiriwa na kushuka kwa thamani ya fedha yake.Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Waziri Mgimwa, ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika wizara hiyo akichukua nafasi ya Mustafa Mkulo, alisema kuwa mpango wa kuirejesha Shilingi ya Tanzania katika thamani yake, unatokana na mfumo mpya ulioigwa kutoka katika mataifa ya Italia, Ugiriki, Ireland na Ureno ambazo zimeamua kuondoa fedha zake kutoka katika matumizi ya Euro na kuhamishia akiba yake kwenda katika Dola ya Marekani.
Majengo pacha ni Benki kuu ya Tanzania Dar Es Salaam.
“Ili kuepuka kuendelea na adha hii, tunapaswa kuhimiza zaidi matumizi yote na mahitaji ya nchi, yafanyike kwa Shilingi ya kitanzania badala ya Dola.Tayari katika hili, Benki Kuu (BoT) imezipa matumaini taasisi za fedha na mabenki kupunguza kiwango kilichokuwa kimeruhusiwa kuweka akiba (deposit) ya fedha za kigeni kutoka asilimia 20 hadi kufikia asilimia 10.”Alisema kupitia mkakati huo, serikali itajikita katika kuuza wa bidhaa nyingi nje ya nchi kuliko uagizaji.Pia alisema serikali itawashauri wawekezaji waliopo nchini na wanaokuja kutumia fedha za kitanzania badala ya dola ili kuimarisha Shilingi.
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen