MBUNGE WA CCM ALIYETELEKEZWA AKARIBISHWA CHADEMA

Mbunge wa Mbarali CCM, Dickson Kilufi, ameshauriwa kukihama chama chake na kujiunga na Chadema ambacho kinatetea wananchi.
Mbunge wa CCM aliyetelekezwa bw.Modestus Kilufi
Ushauri huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, wakati akiwahutubia wananchi wa Rujewa katika wilaya ya Mbarali katika operesheni ya Chadema Twanga Kotekote. Alisema anamshauri Kilufi kuachana na CCM na kujiunga na chama hicho.
MMwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini bw Mwambigija
Alisema anamshauri hivyo kutokana na CCM kutokuwa na sera za kuwasaidia wananchi wa Rujewa kutatua matatizo yanayosababishwa na wawekezaji wanaoonyesha ubabe kwa wananchi wazawa. Alisema wakati Mbunge Kilufi alipokamatwa na polisi na kupelekwa jijini Mbeya na kufunguliwa kesi, hakuna kiongozi yeyote wa CCM aliyejitokeza kumsaidia hata kumwekea dhamana, hali iliyoonyesha kuwa hawamjali wala kumthamini.
Kutokana na hali hiyo, alimtaka Kilufi kujitoa CCM na kujiunga na Chadema na kumuhaidi kuwa akiwa Chadema atapata ubunge kwa kuwa wananchi wanampenda kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi.“Kilufi ni kipenzi cha wana-Mbarali kutokana na utendaji wake wa kazi anaouonyesha hata ukihama chama chako bado utapata nafasi huku kwani wananchi wanaangalia utendaji wako na sio chama,” alisema Mwambigija.
Alisema Kilufi ni mwanaharakati mpigania ardhi wana-Mbarali dhidi ya wawekezaji wanaotaka kuwageuza wananchi manamba wakati nchi iko huru.
Mwambigija alisema: “Kilufi anaimba kama malaika na anacheza kama shetani kwani anasaidia wananchi wakati chama hakina sera ya kusaidia wananchi.”
CHADEMA YAVUNA 138
Mwenyekiti wa CHADEMA na makada wengine wa chama hicho pindi mwenyekiti huyo alipotembelea soko lililoungua la Sido Mbeya.
Hali kadhalika Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata wanachama wapwa zaidi ya 50 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwemo aliyekuwa kada wa CCM kutoka kikosi cha Green Gurd Ayub Mlwilo mkazi wa Lujewa huku wengine 138 wakijiunga na chama hicho.Mavuno hayo ya chadema yalitokana na mkutano mkubwa walioufanya juzi katika maeneo tofauti Wilayani Mbarali ambapo pamoja na masuala mengine kukusanya changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.Akiwapokea wanachama hao wapya Mwenyekiti wa Wilaya Mbeya mjini John Mwambigija alimaarufu Mzee wa Upako,aliwataka wanachama wapya kusoma ilani ya chama na kuielewa ili wasiwe watu wa kuhangaika kwenda vyama vingine visivyokuwa na ilani zinazotekelezeka.
Vyanzo:TZMPAKAAU IPPMEDIA na KALUNGULA
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen