Best Blogger TipsSoon

Samstag, 24. September 2011

TZMPAKAAU

    Rais wa Zambia akubali matokeo(Zambiani president Rupia Banda has accepted the election result)

  • Adai sauti ya wananchi wa Zambia lazima iheshimiwe(He claimed that the voice of most of the citizens must be respected)
  • Ni matokeo machungu(The results has brought bitter experience)


Zambia's Patriotic Front (PF) presidential candidate Michael Sata, center, speaks to journalists after casting his vote in Lusaka, Zambia, Thursday Oct. 30, 2008. Zambians elected a replacement for their president who died in offic
Katikati ni Rais mpya wa Zambia Bw Michael Sata akihojiwa na waandishi wa habari

Bw Sata, aliyegombea urais mara nne, alitangazwa kuwa mshindi usiku baada ya kupata asilimia 43 ya kura zote.

                             Rais wa Zambia aliyemaliza muda wake bw Rupiah Banda

"Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote tusikilize," Bw Banda aliwaambia waandishi wa habari, huku akifuta machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake. 


Zambia

Chama chake cha Movement for Multiparty Democracy kimeongoza Zambia kwa miaka 20.



"Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu, tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna nyingine yeyote ile," Bw Banda alisema.

Siku ya Alhamis, kulikuwa na ghasia eneo la kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.

Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema Bw Banda hatoweza kumfikia Bw Sata.
Sources:TZMPAKAU,BBC

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen