WATOTO WA WAZIRI WAJIUNGA CHADEMA
Watoto wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, wamejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kukabidhiwa kadi za uanachama wa chama hicho jana, jijini Dar es Salaam.
Watoto hao ambao
wanamuita Waziri Wassira baba mdogo, Ester Wassira na Lilian Wassira wote wakiwa ni wanasheria, walikabidhiwa kadi mpya za uanachama na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa.
wanamuita Waziri Wassira baba mdogo, Ester Wassira na Lilian Wassira wote wakiwa ni wanasheria, walikabidhiwa kadi mpya za uanachama na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa.
Akiwakabidhi kadi hizo, Dk. Slaa alisema pamoja na Wassira kupiga makele juu ya Chadema kuwa ni chama chenye vurugu, Watanzania wamegundua kuwa hizo ni propaganda na kitendo cha watoto wake kujiunga na Chadema inaonyesha kuwa wamezikubali sera za chama hicho.
Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu watoto wake kujiunga na Chadema, Wassira alikiri kuwa hao ni watoto wake lakini hana habari za kuwa wamejiunga na chama hicho.
"Kwani ukiwa baba mdogo unafuatilia vyama, sina habari zao kama wamejiunga na Chadema kuna tatizo gani, wameshasomeshwa ni wakubwa ... siwezi kujua labda wanaume zao wapo Chadema sasa nitawazuiaje wasijiunge nao," alisema Wassira.
Alisema bado ana imani kuwa chama hicho kitakufa pamoja na kwamba watoto wa kaka yake wamejiunga na Chadema, hivyo wasubirie kufa na chama hicho na itakuwa bahati yao mbaya.
Wassira alisema yeye hana chuki na Chadema lakini ataendelea kupingana katika hoja kwa kuwa chama hicho kinakwenda kinyume na kanuni.
Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama hao wapya, Dk. Slaa alisema Wassira alikitabiria Chadema kitakufa baada ya mwaka mmoja na kutumia muda mwingi katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV kukiponda badala ya kuzungumzia hoja iliyompeleka.
Alisema mara nyingi Chadema kimekuwa kikionekana chama cha vita na vurugu na hata mauaji yakitokea inaonekana ndio kimehusika lakini sasa wananchi wana uelewa wa kutambua yale wanayoelezwa.
"Wassira alitabiri chama chetu kitakufa na leo watoto wake wamejiunga na Chadema na kwamba ni mara ya kwanza kuwaona sasa sifahamu walipendezwa na chama chetu kuwa ni cha vurugu siamini kama mtu mwenye akili zake timamu atakubali kuingia katika chama chenye vurugu sasa sielewi wamefuata vurugu," alihoji Dk. Slaa
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi zao, Ester kwa upande wake alisema kilichomfanya ajiunge na Chadema ni kutokana na chama hicho kuwa na chachu ya maendeleo.
"Kwa sasa tunahitaji kuona viongozi waadilifu utakuta kiongozi anatolewa katika wizara fulani na kupelekwa wizara nyingine wakati sio mwadilifu imefika wakati wa kubadilika huu ni mfumo wa vyama vingi vya siasa," alisema Ester. Alisema Chadema ni chama chenye watu waadilifu wanaohitaji mabadiliko.
Naye Lilian alisema ameamua kujiunga na chama hicho akiamini kuwa ni chama pekee ambacho kitaweza kufikisha ndoto zake kwani wananchi wanaamini Chadema itawasaidia pale kitakapongia madarakani.
Alisema Watanzania wanatakiwa kuchagua Tanzania mpya kwani Chadema ni chama chenye demokrasia ya kweli na sera zake zinakubalika na ushindani ndio unasaidia kuwepo kwa maendeleo.
Akizungumzia chama chake kukosa nafasi ya Umeya jijini Mwanza, Dk. Slaa alisema uchaguzi ni suala la mahesabu na kwamba ameshindwa kuelewa ni kwanini jiji hilo limegawanyika.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Ippmedia ,Haki Ngowi na Majengwa
Vyanzo:TZMPAKAAU,Ippmedia ,Haki Ngowi na Majengwa
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen