Nchi inapotoka katika hali duni kwenda hali bora zaidi basi ni maendeleo.Maendeleo haya yanaweza kuwa kwenye nyanja muhimu kama makazi ya wananchi wake,upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake,nyanja ya elimu,nyanja ya mifumo mbali mbali ya kijamii kama mifumo ya afya,usafirishaji,uzalishaji na kadhalika.Siku za hivi karibuni kumekuwa na mtizamo ambao mimi naweza kusema mtizamo potofu maeneo mbali mbali duniani na hata Tanzania juu ya maendeleo ya Taifa.Dhana hii inadai kwamba maendeleo ya nchi yanaletwa aidha na rais wa nchi au basi maendeleo ya nchi yanaletwa na chama fulani au hata kundi fulani la wanasiasa.Ni sahihi kuwa rais na serikali kwa maana ya viongozi wa ndani ya serikali wanajukumu kubwa sana katika kusababisha maendeleo ya nchi.Viongozi wa serikali wanaweza kuwafungulia wananchi wao milango ya maendeleo hasa ikizingatiwa kuwa wao ndio wenye nyenzo muhimu na madaraka ya kufanya hivyo .Viongozi wa nchi wanauwezo wa kubadilisha sera za nchi na kuzisimamia ili kufanikisha na kuharakisha maendeleo . Hii ni mifano na labda inatoa picha halisia au la lakini ni mifano, serikali inaweza kupanga na kubadilisha sera za uwekezaji ambapo wanaweza kuongeza kodi kwa wawekezaji wakubwa ili kuongeza pato la taifa kwa ajili kuboresha usafirishaji ndani ya nchi .Serikali pia inaweza kupunguza kodi kwa wawekezaji wadogo ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi wa ndani kwanza, wa nje pia na vile vile kuongeza pato la taifa kwa ajili ya kuboresha maswala ya elimu ndani ya nchi. Au labda serikali inaweza kuweka sera zinazowalazimisha wawekezaji hawa kuwapa kazi wenyeji wengi ili kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja . Lakini pia serikali inaweza pia hata kutumia benki kuu na sehemu ya pato la nchi kuwekeza kwenye nchi zinazozalisha kwa bei nafuu na zilizokua zaidi kiuchumi kuzalisha bidhaa na kuziuza kwa faida ya nchi,hii ni mifano michache sana ya mambo ambayo serikali inaweza kuyafanya kwa urahisi zaidi kuliko mwananchi wa kawaida ili kusababisha na kuharakisha maendeleo ya nchi.Lakini kwa upande mwingine serikali peke yake,rais peke yake na viongozi wa kisiasa peke yao hawawezi kabisa kuiletea nchi maendeleo ni jukumu la kila mtu kuhakikisha anajisababishia maendeleo yake binafsi kwanza kisha kupeleka maendeleo ndani ya familia yake ,jamii yake na baadaye kuliletea taifa lake kwa ujumla maendeleo.
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen