Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 14. Juni 2012

TZMPAKAAU

TANZANIA YAMKAMATA MSHUKIWA WA AL SHABAB(EMRAH ERDOGAN  SUSPECTED TO BE RESPONSIBLE FOR THE BOMB BLAST IN NAIROBI LAST MONTH AND MEMBER OF AL SHABAB HAS BEEN CAPTURED IN TANZANIA)
Emrah Erdogan anayeshukiwa kuwa mfuasi  wa al shabab na gaidi aliyetega bomu liliojeruhi watu 30 mwezi uliopita mjini Nairobi.
Mtu mmoja anayeshukiwa kuwa ana uhusiano na shambulio la mwezi uliopita katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi amekamatwa nchini Tanzania.
Polisi ya Kenya inasema kuwa Emrah Erdogan ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki.
Kenya inadai kuwa alivuka mpaka mapema mwezi Mayi kutoka Somalia ambako alishiriki mapigano kwa niaba ya kundi la Al Shabab.
Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa katika mlipuko ambao wakuu wa Kenya wanasema ulisababishwa na bomu hilo
.
Polisi ya Tanzania imethibitisha kwa BBC kuwa Bw.Erdogan alikamatwa na kuahidi maelezo zaidi baadaya mda mfupi.
Erdogan ni miongoni mwa watu wanne ambao Polisi ya Kenya imekua ikiwasaka tangu kutokea kwa mlipuko huo.
Ilisambaza picha yake na kuomba habari kuhusu mahali alipo.Bw.Erdogan, anayejulikana pia kama Salahuddin al-Kurdi, inaaminika kuwa aliwahi kusafiri kwenda Waziristan huko Pakistan ya kaskazini magharibi mwaka 2010 ambako alijiunga na kundi la wakereketwa wenye imani kali kabla ya kuelekea Somalia mwaka jana, kwa mujibu wa shirika la habari Reuters.

Vyanzo:TZMPAKAAU,The Habari,Michuzi na BBC

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen