DK ULIMBOKA AOKOTWA BUNJU AKIWA AMECHAKAZWA VIBAYA KWA MAPANGA(DK ULIMBOKA ONE OF THE MASTER MINDS ON DOCTORS STRIKE WHICH IS GOING ON CURRENTLY IN TANZANIA HAS BEEN FOUND BADLY WOUNDED TODAY)
Daktari Ulimboka alipokuwa akitoa maoni yake kwenye mkutano baina ya Waziri Mkuu na Madaktari siku zilizopita.
Habari zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa Kiongozi wa mgomo wa madaktari Bw. Steven Ulimboka ameokotwa maeneo ya Mabwepande akiwa amepigwa mapanga na hali yake ikiwa ni mbaya Fullshangwe imepata habari kuwa kulikuwa na gari lililokuwa likipeleka katika hospitali ya TMJ Mikochezi na lilipofika hapo walimhamishia kwenye Ambulance na kumuwahisha hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu.
Daktari Ulimboka kama alivyoonekana baada ya shambulizi(Picha kwa hisani ya watu wa haki za binadamu)
Fullshangwe imewasiliana na Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Kamanda Kenyela hata hivyo ilipokelewa na msaidizi wake ambaye amesema Kamanda Kenyela amebanwa sana na kazi hivyo tumpigie baadae anaweza kuwa na muda mzuri wa kulizungumzia suala hilo, Haijafahamika bado kama wahusika wa shambulio hilo ni akina nani na tutaendelea kuwataarifu kadiritutakavyopata taarifa
Ikumbukwe Dkt. Ulimboka amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha madaktari kugoma ili kutetea maslahi yao ambayo serikali imeshindwa kuyashughulikia au kuyatolea tamko kwa muda mrefu sasa.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Fullshangwe na Tanzania Journalists Alliance (TAJOA)
Ikumbukwe Dkt. Ulimboka amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha madaktari kugoma ili kutetea maslahi yao ambayo serikali imeshindwa kuyashughulikia au kuyatolea tamko kwa muda mrefu sasa.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Fullshangwe na Tanzania Journalists Alliance (TAJOA)
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen