Best Blogger TipsSoon

Montag, 18. Juni 2012

TZMPAKAAU

GESI ZAIDI YAGUNDULIWA  MTWARA
Waziri wa nishati na madini professa S.Muhogo
Jumla ya gesi asili yenye futi za ujazo wa trilioni 20.97 imepatika katika kina cha maji marefu, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospteter Muhongo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana.
Alisema kiasi hicho cha ujazo wa gesi kinajumuisha kisima kilichogunduliwa wiki iliyopita cha Lavani na kampuni ya Statoil ambayo inashirikiana na kampuni ya Exxon Mobil kwenye kitalu namba mbili Mashariki mwa mkoa wa Lindi, takribani kilometa 80 kutoka nchi kavu.

“Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji wa mafuta na gesi asili hapa nchini. Utafutaji huu umejikita zaidi kwenye Bahari ya Hindi kwenye maji ya kina kirefu,” alisema.
Alisema ugunduzi huo umefanyika Mashariki kwa mikoa ya Mtwara  na Lindi.
Aidha, Profesa Mulongo, alisema kampuni ya Petrobras kutoka Brazil nayo ilichimba kisima kimoja mwishoni mwa mwaka jana kwenye kitalu namba tano.
Hata hivyo, alisema kisima hicho kiitwacho Zeta-1 ambacho kilichimbwa hadi kufikia urefu wa meta 3,695 chini ya bahari, kwa bahati mbaya hakigundua mafuta wala gesi asili ingawa dalili zilionyesha kuwa nzuri.
Alisema katika visima vilivyochimbwa kwenye bahari ya kina kirefu, visima saba vimegundulika kuwa na gesi asili.
Alisema kisima kingine (Papa-1) kinaendelea kuchimbwa kwenye kitalu namba tatu na kwamba kinategemewa kukamilika Julai mwaka huu.
Alisema utafutaji wa mafuta ya gesi kwenye bahari ya kina kirefu unagharimu fedha nyingi na kwani kisima kimoja kinagharimu takribani dola za Marekani milioni 100 hadi milioni 150 baada ya gharama za ukusanyaji takwimu za mtetemo.
Pia alisema visima  vitatu vimekamilika ambapo viwili vimegundulika Songo Songo na Magharibi mwa Mtwara.
Alisema kisima kilichokamilika Mei mwaka huu katika Songo Songo kina uwezo wa kuzalisha mita za ujazo milioni 60 kwa siku.
Profesa Muhongo alisema makampuni makubwa duniani ya utafutaji wa mafuta na gesi asili yapo hapa nchini kwa ajili ya kufanya utafiti. 
Vyanzo:TZMPAKAAU na Ippmedia

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen