Makamu wa Rais Dk.Gharib Bilal amewaongoza maelfu ya watanzania waliofurika kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa msanii wa Bongo movies Steven Kanumba pale Leaders Club jijini Dar Es Salaam.Viongozi wengi wa kitaifa na wa vyama vya siasa nao walikuwa miongoni mwa waombolezaji hao.Akizungumza katika mazishi hayo mchungaji aliainisha mambo muhimu mawili ya kuzingatia alisema " Kwanza kufikiria namna ambayo mtu unaweza kutoa mchango katika jamii na kwa taifa mchango ambao hata mauti yatakapofika basi mchango huo ubaki kama kumbu kumbu ,Pili mchungaji huyo alisema "ni muhimu kuishi huku tukiandaa maisha yetu ya baadaye hivyo kuepuka kutenda mambo yasiyo sawa na kuishi tukimkumbuka Mwenyezi Mungu".Steven Kanumba alifariki usiku wa Ijumaa nyumbani kwake Sinza Vatican Dar Es Salaam.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Michuzi na Clouds FM na TV
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen