JE VIONGOZI WANATEKELEZA WAJIBU NA AHADI ZAO?
Hapo asubuhi kwenye gwaride...hivi kiukweli kuna haja ya kuwakagua hao watoto? Roho inaniuma sana kila nikikaa na kufikiria viongozi wetu wa Kiafrika wanapofanya mambo kinyume na matarajio ya wananchi.
Unakuta mzazi unaamka asubuhi kupanga foleni ili kupiga kura kwa kumchagua kiongozi unayetaraji atakuletea mabadiliko katika mfumo wa maisha yako na familia yako,kinyume chake hali inazidi kuwa mbaya zaidi kimaisha.Haipendezi kabisa kuona viongozi wetu wana maisha ya juu na watoto zao wanasoma shule za ada zilizo juu sana huku wakifumbia macho maisha ya walala hoi.
Suala la mfumo bora wa uongozi lazima liangaliwe upya ili kuleta maendeleo na uhakika wa maisha kwa kila mwananchi.huwezi amini kabisa kuna baadhi ya watu wanapolala huwezi kutofautisha kama ni zizi la mifugo au chumba wanalala wanaadamu.kwa mfano mzuri ambao unaweza kuangalia hiyo picha na kupata uhalisia wa mahala wanapolala watoto hao.
Tunakokwenda sio kuzuri kwa taifa la kizazi kijacho,kwani tutapoteza vizazi vyenye akili,tutapoteza vijana wenye nguvu na tutapoteza taifa lenye matumaini kwa kutozingatia mfumo wa uongozi bora.Inabidi vipindi vinavyokuja viongozi wachaguliwe kwa ahadi na makubaliano ambayo wakishindwa waondoke madarakani kwa hiari yao wenyewe bila malumbano.
Inakatisha tamaa sana kila kukicha wananchi kuzungumzia suala moja la uongozi wenye ahadi hewa.Sio kwamba viongozi wote ni waongo ila wengi kati yao ni waongo na wabinafsi,binafsi nasikitishwa na kulionea huruma taifa ambalo halina future kwa kukosa kupata vongozi wenye huruma na wananchi wao.Sitakata tamaa kuomba MUNGU kwa taifa hili kwani najua kila lenye mwanzo lina mwisho.
Vyanzo:Maganga One na TZMPAKAAU
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen