Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 29. März 2012

TZMPAKAAU

KAMPUNI YA URUSI KUCHIMBA URANIUM NAMTUMBO(RUSSIAN COMPANY TO  MINE URANIUM IN NAMTUMBO TANZANIA)

Serikali inatarajia kufungua mgodi wa uranium wa Mkuju
River (Mbamba Bay), katika wilaya ya Namtumbo, mkoani 
Ruvuma kwa kuingia mkataba na kampuni ya Urusi ya ARMZ


 Uranium Holding.

Akipokea taarifa hiyo kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Diana Chilolo, alisema mradi huo unatajia kuunufaisha taifa, kupitia Sheria ya madini ya 2010 na utakuwa mradi mkubwa wa kwanza  wa madini nchini.
Alisema katika mkataba baina ya Serikali na kampuni hiyo,  hakutakuwepo na migogoro ya kutokana na Serikali kujipanga katika malipo ya wakazi wanaoishi karibu na mradi huo.
“Tumeitaka Serikali iwape haki za msingi wakazi wa maeneo hayo, kwa kuwapa fidia ya mali zao, ikiwemo mashamba, nyumba, hatutarajii kuona migogoro ya ardhi inatokea kama Mwadui, Geita,” alisema.

Kwa kutambua madhara ya kiafya kama kansa ya mapafu na kansa zinginezo achilia mbali athari mbaya kabisa za   kimazingira TZMPAKAAU inaupinga mradi huu kabisa.Toa maoni yako....
Vyanzo:TZMPAKAAU,Ippmedia,Wiki na India Talkies

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen