Kushoto ni waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samweli Sitta
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amevunja ukimya na kutema cheche kuhusu suala la kugombea urais katika uchaguzi wa 2015 na kusema kuwa wanaomkataza kuzungumzia suala hilo wameingiwa kiwewe.
Sitta ambaye amekuwa akitajwa kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo, amesema itakapofika wakati wa kutangaza nia yake hakuna mtu atakayemzuia.
Alisema hayo wakati akifungua Bonanza la Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, lililofanyika Msasani Beach.
"Linapoingia suala la Urais kuna watu wanapata kiwewe, wanaposikia ninataka kugombea, lakini hiyo ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa anaruhusiwa kugombea," alisema Sitta.Sitta aliyasema haya kufuatia kauli ya Rais Kikwete inayotaka ,mgombea wa mwaka 2015 sharti awe ni kijana.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Ippmedia na Haki Ngowi
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen