- Ni baada ya kuahirishwa kwa matokeo ya kura Urais
Jeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linaendelea kushika doria kwenye mitaa ya mji mkuu Kinshasa wakati nchi hiyo ikisubiri matokeo ya uchaguzi, ambayo yamesogezwa mbele kwa muda wa masaa 48. Raia wa Kongo waishio ndani na nje wamefanya maandamano wakitaka matokeo yatangazwe haraka, na hii inazusha hofu mpya kwamba hapo baadaye hali inaweza kuripuka zaidi.
Etienne Tshisekedi
Joseph Kabila
Etienne Tshisekedi, mpinzani mkuu wa Rais wa sasa Joseph Kabila amekwisha yapinga matokeo ya awali ambayo yanamweka Kabila katika nafasi ya mbele, akimpita Tshisekedi kwa asilimia kumi ya kura.
sources:TZMPAKAUna DEUTSCHWELLE
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen