Mwanjelwa market got burnt down
- Ni hasara ya mamia ya mamilioni(the loss is estimated to mount to thousands of dollars)
- Wafanyabiashara walia kwa machungu(the salesmen mourn the loss)
- Serikali ajali isihusishwe na mambo ya kisiasa(the government says the tragedy has nothing to do with the politics)
Mmoja wa mashuhuda wa moto huo
Asubuhi ya jana mishale ya saa 9:15 asubuhi, soko la Mwanjelwa upande wa sido lilishika moto na kuanza kuteketea.Moto uliowaka kwa zaidi ya masaa mawili bila kusimama ukisababisha uharibifu mkubwa wa mali za watu.Ikiwa ni miaka michache tu kupita tangu soko hilo la Mwanjelwa lilipoungua tena na kusababisha hasara kubwa.
Kama sio swala la kusikitisha na kukatisha tamaa basi ni kituko cha zima moto ya mbeya ambao tangu moto huo ulipoanza kuwaka wao waliwasili masaa mawili baadaye .Baada ya zima moto hiyo kuwasili eneo la tukio , walionekana kushindwa kufanya lolote lile kutokana na kuwasili na vifaa vibovu.
Haikufahamika mara moja kama kijana huyu alikuwa akiokoa mali zake ama alikuwa akitmka na mali za watu
Umati wa watu waliokuwa wakishuhudia tukio la moto huo bila kujua nini cha kufanya kutokana na polisi kuzuia raia kuudhibiti moto huo
Mama huyu akipiga yowe mbele ya duka lake lililokuwa likiteketea
Watu waliokuwa wakikimbia ili kuokoa roho zao baada ya moto huo kulipuka
Zima moto ya Mbeya ni wanabongo movie yaani sio zima moto ila wasanii waigizaji hapa walikuwa wamekuja na kudai gari na mashine za gari hilo ni mbovu.
Katika sakata hilo inasemekana ni mtu mmoja tu aliyepoteza maisha yake huku mengi yakijiri.Kama wananchi kupambana na mapolisi waliokuwa kwa njia moja au nyengine eneo hilo ili kurejesha hali ya utulivu.Na tukio moja la ajali lililoripotiwa chanzo cha moto huo kwa mujibu wa mashuhuda ni hitilafu ya umeme katika kibanda kimoja sokoni hapo.
Vyanzo:TZMPAKAAU,Mbeya yetu na IPPMEDIA
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen