Best Blogger TipsSoon

Freitag, 2. September 2011

TZMPAKAAU


UTURUKI:ISRAEL SASA KUKOSA BALOZI
Ripoti hii haitobadili lolote katika kusuluhisha mahusiano baina ya Uturuki na Israel. Uturuki iliitaka Israili iombe msamaha kufuatia mauwaji ya wakereketwa tisa waliopanda meli kwenda Gaza kuonyesha moyo wa kuunga mkono juhudi za Palestina mwaka jana.

Uturuki sasa inasema kuwa imemtimua Balozi wa Israili kutoka nchini humo na pia kusimamisha uhusiano wa kijeshi. Israili bado haijatoa kauli yake rasmi juu ya Ripoti ya Umoja wa Mataifa ingawa serikali ya Uturuki bila shaka itaridhika nayo.
Ripoti hiyo inasema kuwa Israili ina haki ya kuzuwia shughuli za Gaza za baharini na kwamba jeshi lake la wanamaji lilichukua hatua za kujihami dhidi ya ghasia kutoka Uturuki kupitia meli ndogo.
Turkey's ambassador to Israel Ahmet Oguz Celikkol, center, is surrounded by Israeli Defense Minister Ehud Barak, left, and Turkish Foreign Minister Ahmet Davutoglu, right, at the start of Barak's one-day visit, to Ankara, Turkey, Sunday, Jan. 17, 2010. (AP)
Balozi wa uturuki nchini israel katikati bw.Ahmet Oguz Celikkol kushoto ni waziri wa ulinzi wa Israel bw Ehud Barak na kulia ni waziri wa mambo ya nje wa uturuki bw. Ahmet Davutoglu

Hata hivyo, kutokana na ufumbuzi kuwa jeshi la Israili lilitumia nguvu ya kupindukia litawapa Waturuki uzito wa kuweza kufungua mashtaka dhidi ya Makamando wa Israili waliohusika na mauwaji.
Wakati eneo zima la mashariki ya kati likiwa katika hali ya taharuki, nchi hizi mbili zitahitaji kuondoa farakano hii. Hilo ni jambo ambalo huenda likachelewa kufikiwa kwa haraka.

Vyanzo:BBC,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen