Best Blogger TipsSoon

Samstag, 27. August 2011

TZMPAKAAU

 MENGI YAIBUKA JUMUIYA YA WAZAZI






Mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi ya CCM, juzi ulinusurika kuvunjika, baada ya baadhi ya wajumbe kushinikiza Mwenyekiti wake, Balozi Athumani Mhina, kujiuzulu.
Tukio hilo lilijitokeza juzi usiku wa manane, kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya CCM.
Shinikizo la kutaka Mhina kujiuzulu linadaiwa kutokana na mwenyekiti huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake hali ambayo imesababisha mawazo ya kuitaka kuifuta.
Hata hivyo, mpango wa huo ulikwama baada ya baadhi ya wajumbe kumkingia kifua ambao walipendekeza kuundwa kwa tume ya kuchunguza sakata hilo.
Aidha, mkutano huo ulipendekeza pia kuundwa kwa kamati tatu za kusadia utekelezaji wa kazi za jumuiya hiyo.
Baadhi ya hadidu za rejea ni kuchunguza tuhuma za kubinafsishwa kwa watu binafsi baadhi ya vitega uchumi vya jumuiya hiyo, bila ridhaa ya Kamati ya Utekelezaji na Baraza Kuu.
Baadhi ya wajumbe walionekana kukasirishwa kwa kiasi kikubwa kuushindwa kuwepo kwa shughuli zozote zinazoonekana wakati wanazo hazina kubwa ya wasomi.
Habari zinasema wajumbe pia Kamati waliitaka kamati ya Utekelezaji kujiuzulu, lakini baadhi ya wajumbe walitadharisha kuwa kutekelezwa kwa jambo hilo kungekiumiza chama.
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Khamis Suleimani Dadi, alisema kuwa kilikuwa kikao cha kawaida na kwamba hakuna jambo lolote kama hilo lililojitokeza.

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen