Best Blogger TipsSoon

Montag, 4. Juli 2011

Uturuki yatambua waasi wa Libya





Uturuki imetambua Baraza la Mpito la Kitaifa kama waakilishi wa kweli wa raia wa Libya.
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema ni wakati sasa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kuondoka.
Uturuki imeahidi kutoa msaada wa dola milioni $200m kwa waasi, hii ni zaidi ya dola milioni $100m walizotangaza kutoa mwezi uliopita.Ukiachilia mbali waturuki Ufaransa imekuwa ikiwadondoshea waasi silaha mbali mbali kutoka angani.Waasi hawa kwa sasa wanakubalika na nchi nyingi za magharibi na katika baadhi ya nchi kama Austria,U.S.A na nyinginezo balozi zao zimekwisha kufunguliwa rasmi. Kukubalika kwa waasi na misaada wanayopatiwa ni jambo linalozua  maswali mengi.

Vyanzo:BBC ,TZMPAKAAU

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen