Kulia ni mkurugenzi mtendaji wa Mkuki na Nyota Walter Bogya na katikati ni mkurugenzi mtendaji wa Haki Elimu Elizabeth Missokia
Kampuni ya Uchapishaji wa Vitabu na machapisho anuai kwa mara ya kwanza imezindua kitabu cha somo la Kemia kilichochapishwa kwa lugha nyepesi ya kiswahili. Kitabu hicho kilichopewa jina la Furahiya Kemia (Enjoy Chemistry) kilichochapishwa kwa ushirikiano na Taasisi ya HakiElimu kimezinduliwa Mei 9, 2012 na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia. Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu alisema ndani ya kitabu hicho wanafunzi wataweza kusoma na kuelewa vizuri somo la Kemia kwa lugha nyepesi ya Kiswahili jambo ambalo linaibua morali ya wanafunzi kuona masomo ya sayansi ni ya kawaida kujifunza kama yalivyo masomo mengine.
Kitabu kilichozinduliwa cha Furahiya Kemia.
Awali akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkuki na Nyota Publishers, Walter Bgoya alisema kitabu hicho kimechapishwa kwa lugha mbili yaani Kiswahili na Kiingereza ili kuwarahisishia wanafunzi kujifunza sayansi ya Kemia kwa lugha mama ya Kiswahili.
Aidha alisema kitabu hicho kimepitiwa na kukubaliwa na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) kwamba kinaweza kutumika kutokana na kuwa na maneno rahisi na sahihi ya Kiswahili ambayo yatawarahisishia wakati wa kujifunza mada anuai za Kemia hasa kidato cha kwanza.
Wazazi na wadau wengine wa elimu wakifurahia kitabu hicho cha Furahiya Kemia kilipokuwa kikizinduliwa katika ukumbi wa Quality Plaza.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Mkuki na Nyota bw.Walter Bogya, aliishukuru taasisi ya HakiElimu kwa kusaidia kuchapishwa kwa kitabu hicho na kuwataka wadau wengine waungane na juhudi hizo za kuinua lugha ya Kiswahili katika matumizi ya kufundishia hata masomo ya sayansi.
Vyanzo:TZMPAKAAU na THE HABARI

Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen