Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 9. Mai 2012

TZMPAKAAU

KAMPUNI YA SEMES MKOMBOZI WA WANAWAKE JIJINI ARUSHA(SEMES COMPANY  HELPS WOMEN IN ARUSHA TO ERADICATE POVERTY)
Meneja masoko wa SEMES  Atupele Elias akionyesha moja ya mashine za kufanyia usafi katika ofisi mbalimbali na numba mjini Arusha.

KAMPUNI ya Semes ya jijini la Arusha imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa  inawaakomboa wanamke wa nchi ya Tanzania  kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali sanjari  na kuwapatia mitaji ili iwawezeshe kujikwamua kiuchumi.Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Elias Seme alipokuwa katika sherehe za kuzindua kikundi cha kampuni hiyo jijini Arusha.Alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa wanawake wanaondokana na hali ya utegemezi kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa kipaumbele katika kuwakomboa kwa kuwapatia mitaji mbali mbali Bw Seme aliongeza kuwa 


Baadhi ya wafanyakazi wa SEMES


SEMES imeshatoa mitaji ya shilingi milioni tano kwa mwaka huu ambapo pia wameweza kuanzisha vikoba kwa  lengo la kukopeshana ili kuboresha maisha yao,Aliongeza kuwa mbali na hayo kampuni hiyo imefanikiwa  kutoa ajira kwa vijana 21 ambapo  lengo halisi ni kuweza kutoa ajira kwa watu 50-60 kwa mwaka .Akielezea changamoto inayoikabili kampuni hiyo alisema kuwa ni pamoja na ushindani wa kibiashara ambapo kumekuwepo na makampuni mengi kutoka nchi ya nje  yanayohusiana na maswala ya  usafi hivyo kuwepo na upinzani    mkubwa.Alitaja mikakati waliyonayo kuwa ni pamoja na kuongeza vitega uchumi zaidi na kujiboresha ili iweze kujiongezea mapato zaidi ili kuwawezesha vijana wengi kujipatia ajira.
Vyanzo:TZMPAKAAU na Fullshangwe

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen