Best Blogger TipsSoon

Donnerstag, 26. April 2012

TZMPAKAAU

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU
KWA SHULE ZA SEKONDARI KONDOA(AIRTEL HAS OFFERED  BOOKS TO THE  CENTRAL TANZANIA SECONDARY SCHOOLS)
Airtel yatoa msaada wa vitabu shule za secondari wilaya ya Kondoa- Dodoma Chini ya mpango wake wa shule yetu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule 4 za sekondari zilizoko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ili kusaidia maendeleo ya elimu wilayani hapo na katika kutoa huduma kwa jamii.
Ofisa Mauzo wa Airtel Kanda ya Kati, Hillary Tarimo (kulia) akimkabithi vitabu vya taaluma, Leonard Cyprian Ngotta (kushoto) Mwalimu wa taaluma Shule ya Sekondari Hurui. 


Makabithiano hayo yalifanyika katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali na shule ya sekondari zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na Sekondari ya Goma, Gubali, Itaswi na Hurui, zote za wilayani humo ambapo wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa vitabu vyenye thamani ya sh. milioni moja kwa kila shule.
Akizungumza katika hafla ya makabithiano Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Kanda ya Kati, Hillary Tarimo alisema” Airtel kwa kupitia programme ya shule yetu imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule za sekondari wilayani Kondoa na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule zitakazokabithiwa.
Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika
kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu
ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza
Tarimo.

Vyanzo:TZMPAKAAU,the habari na africa-internet.com

Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen