Best Blogger TipsSoon

Mittwoch, 25. April 2012

TZMPAKAAU

MKUTANO MKUU WA EAC KUJADILI OMBI LA SUDANI KUSINI(EAC TO DISCUSS THE SOUTH SUDAN PLEAD)
 Katibu mkuu wa EAC Dr.Richard Sezibera

wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajiwa kukutana Arusha, Tanzania, Jumamosi, Aprili 28, katika mkutano maalum utakaojadili pamoja na mambo mengine, mapendekezo ya maombi ya nchi ya Sudan Kusini, kujiunga na jumuiya hiyo.
Nchi zote tano za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi zinatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa siku moja. Maombi ya Sudani Kusini yatafikiriwa ikiwa ni miezi karibu mitano baada ya maombi ya Jamhuri ya Sudani kukataliwa kwa madai ya kutokidhi vigezo vilivyoanzisha mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkataba huo unaeleza wazi kwamba nchi yoyote inayotaka kujiunga na EAC, sharti iwe imepakana na moja kati ya nchi tano wanachama wa EC. Wakati Sudani ya Rais Omar Al-Bashir inawasilisha maombi yake, haikuweza kukidhi matakwa hayo ya kijiografia.Namna pekee ambayo Sudani inaweza kufikiriwa katika maombi yake, ni pale tu Sudani Kusini itakapokubaliwa na wakuu wa EAC kuwa mwanachama, chanzo kimoja cha habari kililiambia Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA).
Vyanzo:TZMPAKAAU na the habari


Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen