- David Jairo aondoka na funguo za Ofisi
Jengo la wizara ya nishati na madini
HUKU Bunge likichunguza madai ya kuwapo fedha zilizogawiwa kwa Wabunge kutoka Wizara ya Nishati na Madini, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayehusishwa na sakata hilo, David Jairo, ameifunga ofisi aliyokuwa akitumia na anayekaimu nafasi yake anatumia moja ya ofisi za makamishina, imefahamka.Maswi anayekaimu nafasi iliyoachwa na David Jairo, anatumia ofisi za aliyekuwa Kamishna wa Madini Dk. Peter Dalaly Kafumu, ambaye sasa ni Mbunge wa Igunga aliyeshinda uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, Jumapili iliyopita.
Bw. David Jairo
Habari zilizothibitishwa na maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini, zimeeleza kwamba ofisi hiyo kwa sasa haitumiwi na Kaimu Katibu Mkuu, Eliakim Chacha Maswi kwa maelezo kwamba bado ina vitu vya Jairo.Vyanzo:TZMPAKAAU na RAIAMWEMA
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen