Best Blogger TipsSoon

Freitag, 14. Oktober 2011

TZMPAKAAU

  TUNATAKA KUJUA CHANZO CHA KIFO WA KADA WETU






Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kinataka kujua sababu ya kifo cha kada wa chama hicho, Mbwana Masoud, ambaye mwili wake uliokotwa katika pori la Magereza, Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, alisema hayo, katika hitima ya kumuombea marehemu huyo.

Alisema watakuwa bega kwa bega na wana Igunga kupeana taarifa ya dalili yoyote itakayoonekana kuhusika na kifo cha kada huyo

Alisema leo ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, Watanzania wanakumbuka na kuenzi yote aliyokuwa akiyapenda na kuyasisitiza, ikiwamo amani na kuhoji “Amani itatendeka vipi bila haki?”


Dk. Slaa alisema haki haikutendeka katika uchaguzi mdogo wa Igunga kwani kulikuwa na vijana wa chama hicho waliotoa taarifa ya rushwa waliyoshuhudia ikitolewa na chama kingine cha siasa, lakini vijana hao ndio waliokamatwa na kupelekwa jela.

“Amani inatumika vipi bila haki? Hebu ona vijana wetu hadi leo wako jela na hawakuwa na kosa lolote. Walichokuwa wamekifanya ni kutoa taarifa ya rushwa, ambayo ilikuwa inafanywa na chama kingine cha siasa,” alisema Dk. Slaa.

Aliipa pole familia ya marehemu na kuitaka kutoendelea kuhuzunika, kwani kila kifo  kimetoka kwa Mungu na kuwa marehemu alifariki wakati akiwa anapigania haki.


Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, alisema yeye atasimama kama mbunge kuhakikisha anajua kilichomuua mtu huyo, kwani jimbo lake limepoteza nguvukazi kwa kuwa marehemu alikuwa ni mtu aliyependa maendeleo.

“Nitachukua nafasi yangu kama mbunge wa jimbo hili. Na nitachuka hatua kuhakikisha kuwa na najua kilichomuua marehemu, kwani amekufa katika mazingira ya kutatanisha,” alisema Mnyika.

Aliongeza: “Mtu hawezi kufa kiholela kiasi kile halafu tukanyamaza kimya. Na tunavyojua kifo siyo jambo la mchezo. Lazima tutamjua aliyehusika na kifo hicho.”

 Naye mtoto wa marehemu Hawa Masoud aliiomba serikali kuingilia kati jambo hilo kwani mpaka sasa haijaonyesha ushirikinao wowote katika familia hiyo.

Vyanzo:TZMPAKAAU na IPPMEDIA




Keine Kommentare:

Kommentar veröffentlichen