Oil spillage in Newzealand

Oil leaks from the grounded MV Rena in Tauranga, New Zealand. The 47,000-tonne Rena, a Liberian container vessel, struck a reef on Wednesday, causing a slick that has spread over 5km. Authorities are preparing for the worst environmental disaster in New Zealand history should the vessel break up and spill 1,700 tonnes of fuel into the Bay of Plenty(mafuta yaliyomwagwa na meli ya MV RenaNewZealand.Meli ya Rena yenye tani 47000 ya Liberia iligonga mwamba jumatano na kusababisha mchirizi wa mafuta unaofikia kilometer 5.Mamlaka za Newzealand zinajiandaa kwa uharibifu mbaya kabisa wa mazingira katika historia ya nchi hiyo kama meli hiyo ikivunjika na kuvujisha tani 1700 za mafuta).


A penguin found on the beach.(Penguin aliyepatikana katika mwambao Tauranga ulioathirika na tukio hili.)

Meli ya MV Arena ambayo inahusishwa moja kwa moja na tukio hili.(MV Arena which is direct concerned with the oil spillage)
Kuna wasiwasi kuwa meli hiyo, iitwayo Rena, inaweza kupasuka katika upepo mkali unaotarajiwa kesho.Meli hiyo imekuwa ikivuja mafuta tangu ilipokwenda mrama siku ya Jumatano.
Meli sita ziko katika eneo hilo kujaribu kuyazoa mafuta hayo, lakini juhudi za kuyayusha mchirizi wa mafuta hazikufanikiwa, na viumbe katika bahari vimeanza kuathirika.
Waziri Mkuu wa New Zeland, John Key amezuru eneo hilo; na aliiambia redio ya taifa kwamba ni muhimu kuchunguza sababu ya ajali hiyo
"Watu wanaujua mwamba huo, na kwa meli kuelekea kwenye mwamba bila ya sababu, usiku, bahari ikiwa shuari, inaashiria kuwa kuna kosa kubwa lilotokea.
vyanzo:TZMPAKAAU,BBC na Gurdian
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen