Wangari Maathai send- off
- Maiti ya Wangari Maathai yachomwa moto kama alivyousia

Kabla ya hapo Bibi Maathai, aliyefariki mwezi uliopita kutokana na saratani, aliagwa kwa maziko ya kitaifa.
Ibada ya wafu ilifanywa kwenye bustani ya Uhuru Park, Nairobi, ambayo Wangari aliitetea sana wakati serikali ya Rais Moi ilipotaka kuruhusu majumba kujengwa katika bustani hiyo.Maelfu ya watu walifurika katika bustani hiyo, wakiongozwa na kiongozi wa Kenya, Rais Mwai Kibaki.Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Makaazi, Bibi Anna Tibaijuka, ambaye piya alikuwa rafiki wa Bibi Maathai.Bibi Maathai aliwahi kupata tuzo ya amani ya Nobel, na alikuwa maarufu kwa kazi yake ya kutetea wanawake na mazingira.
Vyanzo:TZMPAKAAU ,BBC na Positivenewsus
Keine Kommentare:
Kommentar veröffentlichen