Best Blogger TipsSoon

Freitag, 25. Februar 2011

TZMPAKAAU




Maandamano makubwa ya Chadema Mwanza
ajenda kuu zikiwa ni
  • Kupinga malipo ya Tanesco kwa dowans
  • Kuitaka serikali kudhibiti mfumko wa bei
  • Kupinga matokeo na mchakato wa uchaguzi wa umeya jijini Arusha



  Misafara ya waaandamanaji hao kwa karibu zaidi




Jumbe mbali mbali za waandamanaji hao kama zilivyosomeka

Mwisho ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubu halaiki ya wafuasi wa chama hicho

Maelfu ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walifanya maandamano ya amani yaliyoongozwa na viongozi wa juu wa chama hicho, ambayo yalikuwa na msisimko mkubwa bila ya vurugu yoyote.
Maandamano hayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kutoilipa Kampuni ya Dowans, kupanda kwa bei ya umeme na kutokubali uchaguzi uliomweka madarakani meya wa Jiji la Arusha. Maandamano hayo yaliyoongozwa na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilibrod Slaa na wabunge karibu wote wa chama hicho kutoka karibu majimbo yote Tanzania, yalianzia katika viwanja vya shule ya msingi Bugarika na kumalizikia katika viwanja vya Furahisha jijini hapa ikiwa ni karibu ya kilometa 10, ambapo viongozi hao wote walishiriki mwanzo hadi mwisho pamoja na maelfu ya wananchi wa Jiji la Mwanza, Baadhi yao wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano huo mkubwa kwenye viwanja vya Furahisha, Dk. Slaa alisema kuwa Chadema inamtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua kali wale wote walioliingiza taifa katika matatizo ya kampuni ya Dowans.
Alisema kuwa anaamini kuwa kabla ya kumaliza maandamano hayo ya siku tisa katika mikoa tofauti, Kikwete atatangaza kuwachukulia watu hao waliosababisha taifa kutaka kuilipa Dowans wakati kampuni hiyo ni haramu kutokana na Kamati ya Bunge kutamka kuwa mkataba wa Kampuni ya Richmond uliorithiwa na Dowans haukuwa halali.
“Tunajua kabla hatumaliza maandamano yetu ya siku tisa tuna imani kubwa kuwa (Rais) Kikwete atangaza kuwachukulia hatua waliohusika la sivyo wananchi watatumia nguvu ya umma kama nchi za Kaskazini ya Afrika ambako kuna wimbi la nguvu ya umma ambalo linawatoa madarakani viongozi,” alisema Slaa.
Pia aliwaomba wananchi kuwazomea wabunge wote wa CCM watakapokuwa majukwaani kama walivyofanya wakati ule wa EPA, ambapo walikuwa wakiwazomea wabunge kila walipokuwa wakihutubia.
Naye Mbowe pamoja na mambo mengine ya kuishinikiza serikali kupunguza bei ya umeme na kutoilipa Dowans, aliwataka askari wote kuielewa Chadema na kulinda maslahi ya umma badala ya kuwalinda mafisadi wachache wanaoimaliza nchi kila uchao.
“Askari mgome kuwapiga watu, kama Misri askari waligoma kabisa kuwapiga watu, lakini Arusha askari walikubali kuwapiga ndugu zao risasi wakati hawakuwa na hatia,” alisema Mbowe.
Mbowe alimpongeza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, kwa kukubali maandamano hayo na kutowapiga mabomu watu wa Mwanza tofauti na Arusha ambako polisi wa huko kila mara wamekuwa wakiwapiga mabomu wananchi wa huko.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godobless Lema, naye alikuwepo katika maandamano hayo alilaani polisi wa Arusha kuwapiga wananchi kila uchao, ambapo alisisitiza kuwa wananchi wa Arusha sasa hawaogopi mabomu ya machozi na wanayaona kama manukato tu.

vyanzo:Nipashe,chingablog,michuzi

1 Kommentar:

  1. Mambo ya kuficha ukweli ili kulinda heshima za watu wachache yamepitwa na wakati na zaidi ya hapo haya mambo yamelitia Taifa katika hasara kubwa kwa kipindi kirefu.....sasa ni zama za ukweli na ukweli mtupu.Mungu ibariki Tanzania

    AntwortenLöschen